Friday, October 6

MBARONI KWA KUKUTWA NA MIRUNGI

JESHI la Polisi mkoani Morogoro, linawashikilia watu watatu   kwa tuhuma mbalimbali, ikiwamo  kukamatwa na dawa za kulevya aina ya bangi na mirungi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonce Rwegasira, alisema tukio la kwanza lilitokea Septemba 26, mwaka huu  saa 9 usiku eneo la Mikese Mizani wilayani Morogoro Vijijini.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Iddi Juma (42) ambaye ni  dereva na Mkazi wa Tabata-Segerea, Dar es Salaam na Aniset Ferdinand (30) mkazi wa Tabata-Chang’ombe.
Alisema watuhumiwa hao walikamatwa na kupekuliwa na askari waliokuwa doria na kukutwa na bangi viroba 6 inayokadiriwa kuwa na uzito wa kilo 80 wakiisafirisha kwenda Dar es Salaam, ikiwa kwenye gari lenye namba za usajili T438 ARN aina ya Toyota Corsa.
Alisema watuhumiwa pamoja na gari wanashikiliwa na Kituo cha Polisi Mikese.
Katika tukio jingine, Ally Daudi anashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kukamatwa na vichane 27 vya mirungi akiwa amevihifadhi kwenye mfuko wa sandarusi.
Alisema mtuhumiwa alikamatwa Septemba 27, mwaka huu saa 10 jioni eneo  la Vibandani Manispaa ya Morogoro.

No comments:

Post a Comment