Saturday, October 7

Marekani yaiondolea vikwazo Sudan

Rais Omar El Bashir
Image captionRais Omar El Bashir
Marekani imeiondola vikwazo Sudan ikisema taifa hilo la Afrika lilikuwa limeanza kuangazia maswala kuhusu kukabiliana na ugaidi pamoja na ukiukaji wa haki za kibinaadamu dhidi ya raia wanaoishi katika jimbo la Darfur.
Uamuzi wa kuiondolea vikwazo na kusitisha vikwazovya kiuchumi wa taifa hilo unajiri baada ya utawala wa Trump mwezi uliopita kuliondoa taifa hilo katika mataifa ambayo raia wake wamewekwa vikwazo vya kusafiri.
Sudan ndio taifa la pekee ambalo liliondolewa katika orodha hiyo.
Lakini uamuzi huo unaviwacha vikwazo vingine kuendelea kwa sasa ikiwemo vile dhidi ya watu binafsi walio na agizo la kukamtwa kufuatia unyanyasaji uliofanyika katika eneo la Darfur.

No comments:

Post a Comment