Mwendelezo wa zoezi la Upimaji wa Afya Bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye Matatizo ya Macho linaendelea na sasa ni Huduma ya Matibabu ya Macho kwa Wananchi waliobainika kuwa na Matatizo ya Macho kwenye Kampeni ya RC Makonda ya Upimaji wa Afya Bure.
Zoezi hilo ni kufuatia ahadi iliyotolewa na *Jumuiya ya Waislamu wa Dhehebu la Khoja Shia Ithnasheri Jamaat K.S.I.J iliyojitolea kumuunga Mkono RC Makonda kwa kujitolea Matibabu ya wagonjwa watakaobainika kuwa na matatizo ya Macho na Mtoto wa jicho kwenye Kampeni ya Upimaji Afya Bure iliyofanyika Mnazi mmoja.
Zoezi hilo linasimamiwa na *Madaktari bingwa wa Macho kutoka Hospital ya Muhimbili, Hindumandal na Ebrahim Haji.
Kutokana na uhitaji kuwa mkubwa RC Makonda ameomba Taasisi hiyo kupima na kufanya matibabu kwa Wagonjwa 1,000 badala ya 500 iliyoahidi ambapo wameridhia ombi hilo.
Amesema kuwa kwa kawaida *Garama za upasuaji wa Macho ni kati ya Shillingi 900,000 hadi 1,000,000 pamoja na Miwani hivyo kwa Watu 1,000 ni sawa na Kiasi cha Shilling Billion Moja lakini kupitia wadau Wagonjwa hao watapatiwa matibabu na Miwani Bure ili waone Matunda ya Serikali ya awamu ya Tano kupitia RC Makonda.
RC Makonda Anawahimiza Wananchi wenye Matatizo ya Macho kufika kwenye kambi ya matibabu ya Macho iliyopo mtaa wa Hindragand Posta kila Jumamosi na Jumapili kwa kipindi cha Miezi Miwili ili wapatiwe Vipimo, Matibabu na Miwani Bure kwa wenye uhitaji.
Ameshukuru wadau hao kwa kumuunga mkono na kueleza kuwa lengo lake ni kuwawezesha wananchi wasioweza kumudu gharama za matibabu kupata huduma.*
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akiongea na baadhi ya wananchi waliojitokeza katika zoezi la upimaji wa afya bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye matatizo ya macho
Madaktari bingwa wa macho wakimhudumia mwananchi aliyejitokeza katika zoezi la upimaji wa afya bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye matatizo ya macho
Madaktari bingwa wa macho wakimhudumia mwananchi aliyejitokeza katika zoezi la upimaji wa afya bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye matatizo ya macho.
No comments:
Post a Comment