Tanzania ina wataalamu 10 tu, Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) wapo wanane na wengine wawili wanatoa huduma Hospitali ya Bugando Mwanza.
Akizungumza na Mwananchi jana, Mkurugenzi wa Tiba kutoka MOI, Dk Samuel Swai alisema madaktari 10 hawawezi kutoa huduma kwa watu milioni 50.
“Idadi ya madaktari bingwa waliobobea katika upasuaji ubongo ni ndogo ikilinganishwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa dharura hasa wa ajali, tunapokea kwa siku watatu mpaka watano wanaohitaji upasuaji,” alisema Dk Swai.
Dk Swai aliyasema hayo jana baada ya uzinduzi wa mafunzo kwa wataalamu wa upasuaji huo kutoka Ethiopia, Kenya, Uganda, Tanzania na Malawi yanayoendeshwa na Chuo Kikuu cha Weill Cornell kilichopo New York, Marekani
Dk Swai alisema kutokana na uhaba huo wa wataalamu, waliomba kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na hivi sasa tayari wameanza kutoa mafunzo kwa muda wa miaka sita.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji wa Ubongo, Mgongo kutoka Chuo Kikuu cha Weill Cornell, New York Marekani, Dk Roger Hartl alisema kwamba kwa ushirikiano wa miaka 10, Kitengo cha Mifupa MOI kimeboresha matibabu kwa nchi ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment