Wanaume na wanawake kutoka maeneo mbalimbali duniani ambao wamenyanyaswa kijinsia wamekuwa wakisambaza habari zao katika mitandao ya kijamii wakitumia alama ya #Metoo kuonyesha viwango vya unyanyasaji wa kinjinsia ulivyokithiri.
Hatua hiyo inafuatia madai ya unyanyasaji dhidi ya mtayarishaji wa filamu katika Hollywood Harvey Weinstein.
Zaidi ya wanawake 20 akiwemo nyota wa filamu Angelina Jolie, Gwyneth Patltrow na Rose McGowan wametoa malalamishi dhidi yake ikiwemo ubakaji na nunyasaji wa kingono.
Wienstein amesisitiza kuwa uhusiano wa kingono aliokuwa nao ulikuwa umeruhusiwa na pande zote.
Tangu madai hayo kufichuliwa watu wengi maarufu wametumia mitandao ya kijamii kuliangazia swala la unyanyasaji wa kingono huku wengine wakielezea unyanyasaji waliopitia.
Wito huo unaotolewa chini ya #MeToo umetumiwa zaidi ya mara 200,000 tangu Jumapili usiku.
Neno hilo lilipata nguvu baada ya nyota wa filamu Alyssa Milano kuwataka waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono kuwataka waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono kujitokeza ili kuonyesha umoja.
Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii walisambaza habari zao kuhusu vile walivyonyanyaswa.
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Twitter ambaye hakutaka kujulikana alichapisha: Nilikuwa na miaka 19.
Wanaume na watu waliobadili jinsia pia waliunga mkono wito huo akiwemo nyota wa filamu Javier Munoz huku wengine wakisambaza maelezo kuhusu waliyopitia.
Rajini Vaidyanatha
Wito wa #MeToo umesambazwa sana duniani , ikiwemo Uingereza, Marekani , India na Pakistan huku wito mwengine kama huo ukiendelea kusambazwa katika maeneo mengi.
Nchini Ufaransa , watumiaji wa Twitter wanatumia #balancetonporc ama ''rat on dirty old man'' ili kuwashinikiza wanawake kutaja na kuwaibisha washambuliaji wao ,huku #womenwhoroar ni neno jingine linalotumika kuwashinikiza waathiriwa wa unyanyasaji huo kujitokeza na kuongea
No comments:
Post a Comment