Tuesday, October 31

Kiongozi wa upinzani Tanzania Zitto Kabwe aachiwa na kukamatwa tena

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe
Image captionMbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe
Zitto Kabwe , kiongozi mkuu wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha ACT Wazalendo, aachiwa na kukamatwa tena kwa maelekezo ya ofisi ya afisa upelelezi imakosa ya jinai.
Mbunge huyo wa Kigoma mjini, alikamatwa mara ya kwanza asubuhi ya Jumanne nyumbani kwake mjini Dar es salaam na kupelekwa kituo cha polisi Chang'ombe.
Baada ya masaa kadhaa mbunge huyo aliachiliwa huru kabla ya kukamatwa tena.
Akizungumza na BBC, wakili wa Bwana Kabwe, Stephan Ally Mwakibolwa anasema sababu zilizotajwa kwa kushikwa kwake ni kutoa maneno yanayodaiwa kuwa ni ya uchochezi.
"Kauli kubwa haswa wanayosema ni kuihusisha serikali ya CCM na matukio ya watu waliookotwa katika fukwe za bahari ya hindi wakiwa wamefariki ,pamoja na tukio la mbunge Tundu Lissu"
Bwana Kabwe sasa amepelekwa katika kituo cha polisi cha Kamata mjini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment