Friday, October 20

Kenyatta akutana ana kwa ana na jaji mkuu David Maraga

Uhuru akutana na Maraga Oct 20, 2017.
Kwa mara ya kwanza tangu mahakama ya juu ya Kenya kubatilisha uchaguzi wa tarehe nane mwezi Agosti, Ijumaa rais Uhuru Kenyatta alikutana ana kwa ana na jaji mkuu David Maraga wakati wa hafla ya sherehe za kuadhimisha Mashujaa Day kwenye bustani za Uhuru Park mjini Nairobi.
Rais Kenyatta alionekana kumpa mkono jaji huyo na wawili hao wakafanya mazungumzo kwa muda mfupi.
Punde tu baada ya uamuzi huo wa mahakama, Kenyatta, akionekana mwenye gadhabu, alimkosoa Maraga na wenzake huku akitumia maneno ambayo wakosoaji wake waliyataja kama yasiyofaa.
Tume ya IEBC inajitayarisha kwa uchaguzi wa marudio siku ya Alhamisi licha ya muungano wa upinzani Nasa kusema kuwa mgombea wao pamoja na wafuasi wake hawatashiriki kwenye zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment