Tuesday, October 17

Diane Rwigara amwomba Kagame kumuachilia huru Rwanda

RwandaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionDiane Rwigara kiongozi wa upinzani nchini Rwanda
Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda Diane Rwigara amemwomba Rais Paul Kagame kumuachilia huru yeye, mamake na dadake.
Akiwa mahakamani Jumatatu, Bi Rwigara amesema kwamba serikali imefanya jaribio la kuinyamazisha familia yake pamoja na wafuasi wake tangu alipotangaza kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi uliofanyika mwezi Mei mwaka huu.
Wanawake hao watatu, ambao walikamatwa mwezi uliopita, wameshtakiwa kwa makosa ya udanganyifu na uchochezi, tuhuma ambazo wamesema zimechochewa na siasa.
Bi Rwigara alizuiliwa kuendelea na nia yake ya kuwania nafasi ya urais wa Rwanda, Uuhaguzi ambao Bwana Kagame alishinda kwa kishindo kwa karibu asilimia tisini na tisa ya kura zote zilizopigwa.

No comments:

Post a Comment