Sunday, October 29

Cuba yakana kuwashambulia kwa sauti wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani

A car with tourists drives past the US Embassy in HavanaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionCuba yakana kuwashambulia kwa sauti wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani
Cuba inasema kuwa hakujakuwa na mashambulizi ya kutumia sauti dhidi ya wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani kwenye mji wake mkuu Havana, ikisema kuwa madai hayo ni kisiasa yenye lengo la kuharibu uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Cuba Bruno Rodriguez alipinga madai hayo ya kuwepo mashambulizi ya sauti akiyataja kuwa kuwa uwongo.
Marekani inasema kuwa karibu wafanyakazi wake 20 katika ubalozi wake walikumbwa na matatizo ya kiafya na kuwapunguza wafanyakazi wake kutokana na kisa hicho.
Ripot zinasena kwa hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na mashambulizi ya sauti lakini hata hivo hakuna kile kimethibitishwa.
Cuban Foreign Affairs Minister Bruno Rodriguez speaking during a news conference at the Foreign Affairs Ministry in Havana on 3 OctoberHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBw Rodriguez alitaja madai hayo kuwa uongo
Marekani haijailaumu Cuba kwa mashambulizi hayo, na serikali ya Cuba imekana mara kwa mara kuwalenga wafanyakazi wa ubalozi. wa Marekania mjini Cuba.
Marekani iliwatimua wanadiplomasia watano wa Cuba, ikisema kuwa Cuba ilishindwa kuwalinda wafanyakazi wake.
Serikali ya Marekani pia ilifuta shughuli za utoaji visa katika ubalozi wake mjini Havanna
Akizungumza mjini Washington wakati wa mkutana na raia wa Cuba wanaoishi nchini Marekani, Bw. Rodriguez alisema kuwa madai hayo yamesababisha kuharibika kwa uhusiano kati ya serikali hizo mbili.

No comments:

Post a Comment