Saturday, October 7

Chadema chakosoa hali ya uchunguzi wa Tundu Lissu

Mbunge wa Singida mashariki aliyepigwa risasi Tundu Lissu
Image captionMbunge wa Singida mashariki aliyepigwa risasi Tundu Lissu
Chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema kimeuliza maswali mengi kuhusu hatua zilizopigwa katika uchunguzi wa Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu ambaye mwezi uliopita alipigwa risasi mjini Dodoma na sasa amelazwa katika hospitali ya Nairobi kwa matibabu.
Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari , Mkurugenzi mshirikishi na usajili wa chama hicho Benson Kigailia amesema kuwa kufikia sasa hakuna mtu aliyetiwa mbaroni ili kusaidia katika uchaguzi huo.
Kulinaga na gazet la The Citizen Tanzania ,alisema kwamba katika eneo la Kibiti, ambapo mashambulizi na mauaji yamefanyika hatua kadhaa zilichukuliwa ili kuhakikisha kuwa washukiwa wanakamatwa.
Akielezea zaidi , alisema kuwa ni rahisi kwa maafisa wa usalama kuchunguza , kuwatafuta na kuwakamata watu wanaomkosoa rais katika mitandao ya kijamii badala ya kuchunguza na kuwakamata washukiwa wanaotaka kuwaua wengine mchana kutwa.
Gazeti hilo limenukuu akisema kuwa mbali na kuyakamata magari 10 kuhusiana na jaribio hilo la mauaji, la kushangaza ni kwamba hakuna hata mlinzi mmoja aliykuwa kazini katika eneo la Area D mjini Dodoma amekamatwa'', alisema.

No comments:

Post a Comment