Tuesday, October 3

ALIYEMTUSI RAIS MAGUFULI MTANDAONI AHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI 12 AU KULIPA FAINI YA MILIONI TANO


Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
MHASIBU wa Shule ya Sekondari ya St Joseph Cathedral, Elizabeth Asenga leo amehukumiwa kulipa faini ya Sh Milioni tano au kwenda jela miezi 12 baada  ya kukutwa na hatia ya kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais Dk, John Magufuli.
 
Mhasibu huyo anadaiwa kumuita Rais Magufuli  kilaza kupitia mtandao wa WhatsApp.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema mshtakiwa amepatikana na hatia baada ya kuridhika na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na pande wa Jamuhuri kwa kuleta mashahidi saba na kumuona mshitakiwa  ana hatia.

"Upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mshtakiwa umetenda kosa hivyo mahakama  inakutia hatiani kwa makosa uliyoshitakiwa nayo" 

Akimsomea adhabu yake amesema "utatakiwa kulipa  faini ya Sh Milion tano au kutumikia kifungo cha miezi 12 jela," alisema Hakimu Shaidi. 

Kabla ya kutolewa adhabu, mshitakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa mama yake mzazi ni mzee anamtegemea na ana watoto wanaomtegemea.

Hata hivyo, mshtakiwa amelipa faini na amefanikiwa kukwepa kwenda jela

Katika kesi ya msingi, inadaiwa   Agosti 6, mwaka jana mshtakiwa huuo aliwasilisha maneno kinyume cha sheria kupitia mtandao wa WhatsApp katika group la wafanyakazi la STJ kwa nia ya kumtusi Rais.

Mshtakiwa alinukuliwa kuwa "Habari za asubuhi humu hakuna rais kilaza kama huyu wetu duniani angalia anavyompa Lissu umashuhuri,  fala yule picha yake ukiweka ofisini  nuksi tupu ukiamka asubuhi ukikutana na picha yake kwanza siku inakua ya mkosi mwanzo mwisho." 

No comments:

Post a Comment