Mgonga huyo maarufu kama Babu Karatu ameelezwa kuwa alikuwa akishirikiana kutenda vitendo hivyo na mtoto wa mdogo wake aitwaye Abdallah Yahaya (31).
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumamosi, kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Isaya Mbughi amesema mtuhumiwa anadaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Desemba mwaka jana, hadi Oktoba mwaka huu.
Amesema kuwa mwathirika mmoja mwenye umri wa miaka saba siku ya Oktoba 16 mwaka huu saa 11.45 jioni wakati akiogeshwa na mama yake alilalamika kuwa anasikia maumivu makali katika sehemu yake ya siri.
Amesema baada ya binti kuyo kulalamika kwa mama yake mama huyo aliweza kumchunguza kwenye sehemu zake za siri na kubaini kuwa michubuko inayotokana na kuingiliwa kimwili.
“Mama huyo baada ya kuona michubuko hiyo kwenye sehemu za siri za binti yake alimhoji mtoto wake na mtoto huyo aliweza kumtaja mganga wa kienyeji Karatu. Mwaathirika huyo alienda mbele zaidi na kumweleza mama yake kuwa si yeye pekee hufanyiwa vitendo hivyo, bali wapo watoto wengi wamefanyiwa.”
Kaimu kamanda huyo amesema baada ya hapo mama huyo alitoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa wa Minga na kisha yeye na mwenyekiti wa mtaa waliweza kuongozana hadi kituo cha kati cha polisi mjini hapa.
“Jeshi la polisi liliweza kuwakamata watuhumiwa hao ambao wanaishi katika nyumba moja, kwa tuhuma ya ubakaji. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa watoto waliofanyiwa unyama huo wanasoma katika Shule za Msingi Singidani, Nyerere na Mughanga,” amesema.
Mbughi amesema mbinu iliyokuwa inatumika kuwanasa watoto hao wa ni kuwarubuni na kisha kuwaonyesha video/movie, kwenye kompyuta mpakato.
“Wakati watoto hao wa kike wakiendelea kuangalia video sebuleni, mtuhumiwa huyo alikuwa akichomoa mmoja na kuingia naye chumbani na kumwingilia kimwili. Wachache alikuwa akiwachezea sehemu zao za siri. Baada kuingiliwa kimwili watoto hao walikuwa wakipewa zawadi ya shilingi mia mbili au shilingi 2,000,” amesema.
No comments:
Post a Comment