Kwa mujibu wa Udart, mvua iliyonyesha Jumatano Oktoba 25 na Alhamisi Oktoba 26,2017 imesababisha mabasi 29 ya kampuni hiyo kuharibika.
Mwandishi wa Mwananchi ameshuhudia leo Jumatatu Oktoba 30,2017 asubuhi abiria wakitumia nguvu kupanda mabasi ili kuwahi kwenye shughuli zao.
Waliokuwa wakihangaika zaidi ni wanafunzi wa kidato cha nne ambao wameanza mitihani yao ya Taifa leo.
Baadhi ya vituo ambavyo abiria wamekuwa wakigombea mabasi ni vya Kimara, Mbezi na Ubungo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ameshaagiza watoa huduma ya mabasi hayo kuhakikisha yaliyoharibika yawe yametengenezwa ifikapo Alhamisi Novemba 2,2017 ili kuwaondolea adha abiria.
No comments:
Post a Comment