Tume ya uchaguzi nchini Kenya imetangaza kundi la watu sita ambalo litasimamia uchaguzi wa urais wa tarehe 17 mwezi Oktoba katika hatua inayoonekana kuwatenga maafisa wakuu wa tume hiyo.
Wale waliotengwa ni mkurugenzi mkuu wa tume hiyo Ezra Chiloba, naibu wake Betty Nyabuto, mkurugenzi wa usajili wa wapiga kura pamoja na mkuu wa operesheni za uchaguzi Immaculate Kasait, naibu wake Mwaura Kamwati , mkuu wa operesheni za tume hiyo na mkuu wa teknolojia James Muhati.
''Katika uwezo wangu mimi kama afisa mkuu wa uchaguzi wa urais, nimewachagua maafisa wafuatao kuhudumu katika kusimamia uchaguzi wa urais utanaofanyika tarehe 17 mwezi Oktoba 2017'', alisema mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati.
Atakayesimamia mahala pake Ezra Chiloba ni Marjan Hussein Marjan ambaye alikuwa naibu wake na alisaidia kusimamia miundo mbinu katika tume hiyo.
- Uhuru Kenyatta: Tuheshimu matokeo
- Rais Uhuru Kenyatta aionya mahakama
- Chama cha mawakili Kenya chamkosoa Uhuru Kenyatta
- Uhuru Kenyatta: Idara ya mahakama ina 'tatizo'
Bwana Marjana ambaye sasa atakuwa mshirikishi katika uchaguzi huo aliongoza tume hiyo katika eneo la Bomas , ambacho ndicho kilichokuwa kituo kikuu cha kuhesabu kura cha tume hiyo kupokea fomu za matokeo za 34B kutoka katika maeneo bunge.
Wadhfa wake bi Nyabuto umechukuliwa na Dkt Sidney namulungu ambaye atakuwa kiongozi wa operesheni huku kazi ya bi Kasait na bwana kamwati ikichukuliwa na bi nancy kariuki ambaye ataongoza kitengo cha mipango
- IEBC yasema mfumo wake haukudukuliwa Kenya
- Odinga: Mitambo ya tume ya uchaguzi ilidukuliwa
- Kamishna wa tume ya uchaguzi Kenya azuiwa Uwanja wa ndege
Katika mabadiliko hayo bwana Chebukati alimbadilisha bwana Muhati na Albert Gogo.
No comments:
Post a Comment