Wednesday, September 6

Australia kuwalipa wahamiaji dola milioni 55 kama fidia

Wahamiaji hao wote walipelekwa katika kituo kilichopo Manus walipokuwa wakijaribu kuingia nchini humo.
Image captionWahamiaji hao wote walipelekwa katika kituo kilichopo Manus walipokuwa wakijaribu kuingia nchini humo.
Hakimu mmoja nchini Australia amepitisha malipo ya zaidi ya dola milioni hamsini na tano kama fidia kwa wahamiaji waliokuwa wanashikiliwa na wanaoshikiliwa mpaka hivi sasa nje ya kituo cha kushikilia watu kilichopo katika kisiwa cha Manus.
Zaidi ya watu elfu moja mia tatu waliokuwa wanaomba hifadhi na wakimbizi watapokea malipo hayo, kama sehemu ya makubaliano nje ya mahakama na serikali yaliyofanyika mwanzoni mwaka huu.
Wahamiaji hao wote walipelekwa katika kituo kilichopo Manus baada ya kujaribu kuingia nchini humo.
Wanasema walizuiwa kinyume cha sheria hivyo kupata matatizo ya kisaikolojia na kimwili.
Wengi wa wanaoshikiliwa wanatoka nchini Iran, Iraq na Afghanistan.
Kituo hicho kitafungwa mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment