Friday, September 1

waasi wa FARC Colombia wabadili mwelekeo

Colombia
Image captionWaasi wa zamani wa Colombia, Farc wametangaza jina lao jipya
Waasi wa zamani wa Colombia, Farc wametangaza jina lao jipya na kuonesha hadharani nembo yao mpya huku wakielekea ukingoni mwa kikao huko Bogota ili kuwachagua wawakilishi wao kushika jukumu jipya kama chama cha siasa.
Harakati za waasi hao wa zamani zitahifadhi jina lake maarufu, Farc, ingawa kifupi cha jina lake kitawakilisha mantiki tofauti katika lugha ya Ki Hispania, ambayo inatafsiriwa kama Nguvu mbadala ya mapinduzi kwa Watu wa kawaida.
Nembo ya chama hicho cha kisiasa itakuwa ni ua la waridi jekundu. Chini ya makubaliano ya amani yaliyotiwa saini miaka uliyopita pamoja na upande wa serikali, waasi hao wa zamani wamehakikishiwa angalau viti kumi katika uchaguzi wa makongamano mwaka ujao na pia mwaka 2022.

No comments:

Post a Comment