Gavana wa Florida ametangaza hali ya hatari baada ya kimbunga Irma kuonekana kujiimarisha zaidi.
Irma kinaonekana kuelekea pande za Mashariki mwa visiwa vya Caribbean na kinatarajiwa kuingia Florida siku ya Jumatano.
Kinatarajiwa kupiga sehemu kadhaa za visiwa vya Caribbean vikiwemo Leewards, Haiti na kisiwa cha Marekani cha Puerto Rico, kabla ya kuelekea Florida.
Irma kimepata nguvu na upepo unaovuma kwa kasi ya kilomita 215 kwa saa, na kinatarajiwa kupata nguvu zaidi ndani ya saa 48 zinazokuja.
Kimbunga hicho kinakuja wakati wenyeji wa majimbo ya Texas na Louisiana wakikadiria athari za kimbunga Harvey, ambacho kilisababisha mvua kubwa na kuharibu maefu ya nyumba.
Hata hivyo kituo cha vimbunga cha Marekani kinasema kuwa ni mapema sana kutabiri njia kitapitia Irma au athari zake kwa Marekani.
Gavana Scott Fox anataka kuwapa mamlaka za mji wake muda wa kutosha kujiandaa kabla ya kimbunga hicho.
Hivi karibuni kimbunga kikali cha Hurricane Harvey kilipiga majimbo ya Texas na Louisiana huku kikiacha madhara mengi sana.
Irma kilitarajiwa kuwasili visiwa vya Leeward, mashariki mwa Puerto Rico baadaye Jumanne au mapema Jumatano.
Kinaweza kusababissha mvua ya hadi sentimita 25 katika sehemu kadha za kusini na kusababisha maji kupanda hadi mita 3 kuliko viwango vya kawaida.
Puerto Rico pia imetangaza hali ya tahadhari. Gavana Ricardo Rossello alitangaza kufunguliwa kwa makao ya dharura yanayoweza kuwahifadhi hadi watu 62,000.
No comments:
Post a Comment