Wednesday, September 13

Uturuki yanunua mfumo wa kujilinda na makombora kutoka kwa Urusi

Mfumo wa kujilinda na makombora kutoka Urusi S-400
Image captionMfumo wa kujilinda na makombora kutoka Urusi S-400
Uturuki imetia saini makubaliano yaliogubikwa na utata na Urusi kulihami jeshi lake na mfumo wa kudungua makombora wa S-400.
Rais Reccep Tayyip Erdogan alisema kwamba Ankara tayari imetoa malipo ya kwanza ya mkataba huo unaotarajiwa kugharimu $2.5b.
Uturuki ina jeshi la pili kwa ukubwa katika muungano wa NATO.
Washirika wa muungano huo wa majeshi ya kimataifa wametakiwa kununua mifumo ya hali ya juu ya kujilinda dhidi ya makombora.
Uturuki imekuwa ikiimarisha uhusiano na Urusi baada ya ushirikiano wake na Marekani kuzorota
Image captionUturuki imekuwa ikiimarisha uhusiano na Urusi baada ya ushirikiano wake na Marekani kuzorota.
Uturuki imekuwa ikiimarisha uhusiano na Urusi baada ya ushirikiano wake na Marekani kuzorota.
Urusi inasema kuwa mfumo huo wa kujilinda dhidi ya makombora unaweza kubaini kombora lililopo umbali wa kilomita 400 na unaweza kudengua hadi makombora 80 kwa mpigo, ukilenga makombora mawili kila awamu.
Uturuki imekuwa ikipinga mpango wa Marekani kuwaunga waasi wa Kikurdi nchini Syria ambao wanahusishwa na waasi wa kikurdi nchini Uturuki.
Rais wa Uturi Reccep Tayyip Erdogan na mwenzake wa Urusi Vladmir PutinHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais wa Uturi Reccep Tayyip Erdogan na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin
Urusi iliweka mfumo huo karibu na kambi yake ya kijeshi katika eneo la Latakia nchini Syria mnamo mwezi Disemba 2015 baada ya ndege ya kijeshi ya Uturuki kudengua nedege ya kijeshi ya Urusi Su-24 katika mpaka wa Uturuki na Syria.
Kisa hicho kilisababisha mzozo wa kidiplomasia kati ya Urusi na Uturuki, lakini rais Erdogan baadaye alisitisha mgogoro wake na rais Vladmir Putin.
Mshauri wa kijeshi wa rais Putin, Vladmir Kozhin alisema kuwa makubaliano hayo na Uturuki yanatokana na maslahi ya Urusi.
''Unaweza kuelewa hali ilivyo ambapo baadhi ya mataifa ya magharibi yamekuwa yakiitishia Uturuki''.

No comments:

Post a Comment