Wednesday, September 13

Korea Kaskazini: Tutailetea Marekani machungu makubwa

North Korean leader Kim Jong-un at an undisclosed location, released 3 September 2017Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKorea Kaskazini inasema imeunda na kulifanyia majaribio bomu la haidrojeni
Korea Kaskazini imetishia Marekani na kusema kuwa itasababisaha machungu makali ambayo Marekani haijawai kushuhudia kufuatia vikwazo vipya vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa.
Mjumbe wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa ameishutumu Marekani kwa kutafuta makabiliano ya kisiasa , kiuchumi na kijeshi.
Mapema Marekani iliapa kuweka shinikizo zaidi ikiwa Korea Kaskazini itaendela na njia zake hatari.
North Korea's intermediate-range strategic ballistic rocket Hwasong-12 lifting off from the launching pad at an undisclosed location near Pyongyang, 30 August 2017Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKorea Kaskazini imekuwa ikifanyia majaribio makombora yake
Vikwazo vya Umoja wa Mataifa ni hatua ya kuhakikisha kuwepo uhaba wa mafuta na kipato kufuatia mipango yake ya nyulia.
Hatua hizo zinapiga marufuku uuzaji mafuta kwenda Korea Kaskazini na uuzuaji wa bidha kutoka Korea Kaskazini baada ya jaribio la sita na kubwa zaidi la bomu la nyuklia mapema mwezi huu.
Han Tae Song, ambaye ni balozi wa Korea Kaskazini kwenye Umoja wa Mataifa alisema amekataa kile alichokitaja kuwa vikwazo vilivyo kinyume na sheria.
"Hatua zitazochukuliwa na Korea Kaskazini zitaisababishia Marekani machungu makali ambayo hajawai kushuhudiwa katika historia yake," aliambia mkutano huko Geneva.
Nikki Haley, United States ambassador to the United Nations, raises her hand as she votes yes to levy new sanctions on North Korea designed to curb their nuclear ambitions during a meeting of the United Nations Security Council concerning North Korea at UN headquarters, 11 September 2017 in New York City.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUmoja wa Mataifa umeiwekea vikwazo mara kwa mara Korea Kaskazini

No comments:

Post a Comment