Kiongozi wa Myanmar Aung San Suu Kyi amesema kuwa serikali yake haina hofu ya kuchunguzwa kuhusu njia inashughulikia suala la watu wa Rohingya.
Ilikuwa hotuba yake ya kwanza kwa nchi kuhusu ghasia katika jimbo la Rakhine ambazo zimesababisha zaidi ya watu 400,000 wa jamii ya Rohingya kuvuka mpaka na kuingia nchini Bangladesh.
Bi Suu Kyi amelaumiwa vikali kuhusu jinsi alishughulikia suala hilo.
Lakini amesema kuwa waisilamu wengi hawajakimbia jimbo hilo na kwamba hali imetumia
- Myanmar yatakiwa kukoma kuwatesa Waislamu wa Rohingya
- Wapiganaji wa Rohingya watangaza kusitisha mapigano, Myanmar
Kwenye hotuba yake kwa bunge la Mynammar, Aung San Suu Kyi alisema amuhusuniswa na kuendelea kutaabika kwa watu wote katika mzozo huo na kwamba Myanma imejitolea kutatua suala hilo kwa jamii zote nchini humo.
Bi Suu Kyi ambaye ameamua kutohudhuria mkutano wa baraza la Umoja wa Mataifa mjini News York badaye wiki hii, alisema kuwa alikuwa anataka jamii ya kimataifa kufahamu kile kilichokuwa kikifanywa na serikali yake.
No comments:
Post a Comment