Saturday, September 2

Paa afanya uharibifu katika nyumba ya maiti Australia

PaaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPaa (si aliye pichani) alisababisha uharibifu mkubwa wa kuta na samani za nyumba ya kuhifadhia maiti
Chumba cha Australia kimeachwa "kikiwa katika hali mbaya zaidi" baada ya uharibifu uliotekelezwa na Paa ndani yake na kukimbia kimbia kila mahali kwa muda wa dakika 20, kimeelezea kituo hicho.
Mnyama huyo alipasua madirisha ya kituo hicho kabla ya kuwafukuza wahudumu katika jengo hilo mjini Melbourne siku ya Alhamisi, kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa kituo hicho James MacLeod.
Mara Paa huyo alipoingia ndani , aliharibu samani na kuta kabla ya wahudumu kuweza kumdhibiti ndani ya chumba kimoja.
Wataalam wa masula ya wanyama pori walimuhamisha mnyama huyo ambaye alikuwa amejeruhiwa, kulingana na polisi.
Bwana MacLeod amesema ilichukua ilibidi wahudumu sita wa wanyamapori waingilie kati kumuondosha Paa huyo kutoka katika kituo cha mazishi cha Tobin Brothers kilichopo kwenye kitongoji cha Ringwood.
"Siwezi kuamini uharibifu ambao umefanyikakatika kipindi cha dakika 20 ," alikiambia kituo cha redio cha 3AW.
"vifaa, mazulia, kuta na samani - vyote vinahitaji kubadilishwa mara moja."
Shirika la habari la Australian Associated Press limeripoti kwamba uharibifu uliofanywa na Paa huyo unakadiriwa kuwa sawa na dola $100,000.
" Hakuna yeyote aliyejeruhiwa wakati wa tukio hilo," ilieleza taarifa ya polisi.

No comments:

Post a Comment