Saturday, September 2

Jiwe kubwa sana kupita karibu na dunia

Map showing path of Asteroid Florence
Jiwe kubwa zaidi kuwahi kupita karibu na dunia katika kipindi cha karibu karne moja linatarajiwa kupita karibu na sayari ya dunia umbali wa karibu maili milioni 4.4 , kimesema kituo cha masuala ya anga za juu cha Marekani, Nasa.
Vipimo vya Florence vilikadiria umbali wa maili 2.7 sawa na kipenyo cha 4.4 na kwamba jiwe hilo halina tisho kwa dunia kwa karne zijazo
Mawe mengine yaliyowahi kupita karibu na dunia, yalikadiriwa kuwa ni madogo sana.
Mawe hayo ambayo yana umbo la vifusi upande wa kushoto ni masalia yaliyobaki wakati wakuundwa kwa jua na sayari.
Jiwe la Florence - lililogundulika mnamo mwaka 1981- linaweza kuwa mara 18 ya wastani wa umbali baina ya dunia na mwezi.
"Florence ni jiwe kubwa zaidi kuwahi kupita karibu na dunia yetu tangu kuanzishwa kwa mpango wa shirika la anga za mbali la Marekani NASA wa kuchunguza na kubaini mawe yaliyopo karibu na dunia ," Amesema Paul Chodas, meneja wa kituo cha NASA kinachochunguza vitu vilivyopo karibu na dunia katika taarifa yake.
Ugunduzi wa mwaka 2017 ni wa jiwe la angani lililopo karibu tangu mwaka 1890 na ukaribu huo hautawahi kutokea hadi baada miaka 2500, shirika la masuala ya anga la Marekani limeongeza.
Mpango wa wanasayansi kuchunguza ukaribu wa jiwe, kwa kutumia mtambo wa rada wa ardhini unafanyika California na Puerto Rico.
Wataalam wa anga za juu pia watakuwa wakilichunguza jiwe hilo yamesema majarida ya masuala ya anga ya Sky na Telescope.
Jiwe ni rahisi kuliona kwa kutumia kifaa cha uchunguzi , si kwa sababu tu ni kubwa , lakini pia kwa sababu huakisi 20% ya mwanga wa jua ambao huchoma kwenye sehemu yake ya chini.
Kinyume chake mwezi huakisi wastani wa 12% pekee.
Kitu chenye ukubwa wa Florencekinaweza kuwa na athari ya kugonga dunia. Wanasayansi wanaamini kuwa sasa wamebaini zaidi ya 90% ya miamba ya aina hiyo ya kutisha inayopita angani karibu na sayari yetu.

No comments:

Post a Comment