Richard Makungwa, ofisa mkuu wa idara ya wateja wakubwa na Serikali wa NMB amesema wametoa fedha hizo kuunga mkono jitihada za Alat na kuiwezesha iwajibike ipasavyo kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
"Halmashauri zipo karibu na wananchi ambao sisi tunawahudumia, kwa hiyo mchango wetu unalenga kuona malengo waliyopanga yanafikiwa," amesema.
Makamu Mwenyekiti wa Alat, Steven Mhapa amesema pamoja na mambo mengine, mkutano huo utahimiza halmashauri zote kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo.
"Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais John Magufuli, mkutano huu utawahusisha pia wakurugenzi wote wa halmashauri za wilaya, majiji na manispaa nchini," amesema.
Amesema katika mkutano huo watatumia siku moja kuzungumzia mamlaka mpya iliyoundwa kwa ajili ya masuala ya barabara za miji na vijiji kutokana na umuhimu wake katika ukuaji wa uchumi.
No comments:
Post a Comment