Monday, September 4

Mtekaji watoto Arusha, Geita anaswa

Kamanda wa polisi mkoani Geita, Mponjoli 

Kamanda wa polisi mkoani Geita, Mponjoli  Mwabulambo 
Polisi Mkoani Geita wanamshikilia  kijana Samson Petro (18) mkazi wa Katoro wilayani Geita mkoani hapa Kwa tuhuma za kuteka watoto katika mikoa ya Arusha na Geita
Kijana huyo amekamatwa usiku wa Septemba 2 ,saa mbili usiku katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungulu iliyopo mji mdogo wa Katoro.
Kamanda wa polisi mkoani hapa , Mponjoli  Mwabulambo amethibitisha kukamatwa Kwa kijana huyo na kusema polisi linaendelea na uchunguzi na utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment