Mary Majaliwa alisema hayo juzi alipozungumza na wahitimu 166 wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Martin Luther kwenye mahafali ya 10 yaliyofanyika shuleni hapo katika mji wa Dodoma.
“Ninawapongeza wanafunzi wanaohitimu, lakini ni lazima mtambue kwamba huu si mwisho wa safari yenu ya masomo kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi. Kwa hiyo muongeze bidii hadi mfike elimu ya vyuo vikuu,” alisema Mary ambaye alihudhuria mahafali hayo kama mzazi kutokana na mtoto wake kuwa miongoni mwa wahitimu.
Katika taarifa iliyotolewa jana na ofisi ya Waziri Mkuu ilimnukuu Mama Mary akiushukuru uongozi wa shule hiyo na walimu kwa malezi mema wanayoyatoa kwa watoto.
Alisema mafunzo yao yanadhihirika miongoni mwa watoto kwa jinsi walivyolelewa kimwili, kiroho na kiakili. “Mtoto wangu nilimleta akiwa na miaka mitano, ameanza elimu ya chekechea na sasa anahitimu darasa la saba. Sasa amekuwa na hofu ya Mungu, anatambua mema na mabaya, tunawashukuru sana.”
Wanafunzi wa darasa la saba nchini wanatarajiwa kufanya mtihani wa Taifa, Jumatano na Alhamisi wiki hii.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene alisema Serikali imekuwa ikitoa Sh22.2 bilioni kila mwezi ili kuboresha elimu ya msingi na sekondari.
Simbachawene aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo kwa niaba ya Waziri Mkuu alisema Serikali itaendelea kuboresha elimu ya sekondari kwa kuajiri walimu wengi zaidi wa masomo ya sayansi. “Wazazi wa wanafunzi wanaohitimu tunawakaribisha kwenye shule za sekondari kwa sababu zote zina walimu wa kutosha, madawati na vifaa vya kufundishia. Kila mwezi tunatenga Sh22.2 bilioni kuendesha shule za msingi na za sekondari hadi kidato cha nne,” alisema.
Simbachawene alisema sasa baadhi ya shule za Serikali zinakabiliwa na changamoto ndogo ya upungufu wa walimu wa sayansi aliyoahidi kuitatua hivi karibuni kwa sababu vibali vya ajira vimeanza kutolewa.
Aliwataka wanafunzi wanaojiandaa kufanya mtihani wasiwe na hofu kwa kuwa kufanya hivyo ni chanzo cha kuchanganya mambo na kisha kufeli.
Mkurugenzi wa shule hiyo, Rabbiely Mmanga aliwaasa wazazi akiwaomba wasiwaingize watoto kwenye migogoro yao kwa kuwa matendo hayo huwaathiri kisaikolojia hata wawapo shuleni.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Gilbert Nhuguti alisema kwa zaidi ya miaka mitano imekuwa na rekodi ya kufanya vizuri kiwilaya na kimkoa kwa kushika nafasi za kwanza.
Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde aliwataka wahitimu watambue wanapohitimu elimu ya msingi, wamejengewa msingi imara.

No comments:
Post a Comment