Polisi mjini Berlin wamemsifu mkimbizi wa Iraqi aliyekabidhi pochi aliyoipata ikiwa na kitita cha dola $16,800.
Pochi hiyo iliachwa ndani ya treni Ijumaa iliyopita usiku na mwanamke kikongwe mmoja mwenye umri wa miaka 79.
Muda mfupi baada ya kuiacha pochi yake , aligundua kosa lake na kuwaarifu maafisa wa mamlaka ya usafiri wa relilakini hawakuweza kuipata pochi hiyo.
Aliyeipata ni mwanafunzi wa miaka 16 kutoka Iraqi , ammbaye alimuarifu mama yake . Siku mbili baadae waliikabidhi pochi hiyo kwa Polisi wa Berlin Jumanne.
Polisi wali Tweet wakimpongeza mvulana huyo.
"Mwanafunzi alipata pochi ikiwa na Euro €14,000 na akaikabidhi kwa polisi. Mmiliki wa pesa amefurahi. Tunasema vizuri sana na asante ,"iliandikwa Tweeter ya polisi.
Familia yake ambayo inaishi katika kituo cha kuwapokea wakimbizi, huenda ikazawadiwa kwa uaminifu wao, kulingana na vyombo vya habari vya Ujerumani.
Chini ya sheria ya Ujerumani, zawadi anayopaswa kupewa mtu aliyeokota kitu ama pesa ya mtu ni asilimia tatu ya thamani yake. Kulingana na sheria hii familia ya mtoto huyo inaweza kupata zawadi ya €210.
No comments:
Post a Comment