Monday, September 4

Merkel asema Uturuki haiwezi kuingia Umoja wa Ulaya

Baada ya mdahalo huu, Merkel ameonekana kumpita wazi Schulz
Image captionBaada ya mdahalo huu, Merkel ameonekana kumpita wazi Schulz
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa anaamini kuwa Uturuki haiwezi kuingia kwenye umoja wa ulaya na kusema kuwa atahakikisha anasisitiza kutokuwepo kwa mazungumzo ya kukubaliwa Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Markel ambae anawania kushinda muhula wa nne katika uchaguzi utakaofanyika mwezi huu amezungumza hayo katika mdahalo na mpinzani wake Martin Schulz ulioonyeshwa kwenye televisheni.
Mahusiano kati ya Berlin na Ankara yameingia mashakani baada ya raia wa ujerumani kuwekwa kizuizini nchini Uturuki.
Mdahalo huo ulikijita katika suala la maelfu ya wahamiaji waliongia ujreumani.
Merkel alionekana kuungwa mkono na wengi alipowasili kwenye mdahalo
Image captionMerkel alionekana kuungwa mkono na wengi alipowasili kwenye mdahalo
Markel alikubali kuwa kuna mafunzo aliyoyapata.
Schulz alimshutumu markel kwa kushindwa kutafutu suluhu.
Kura za maoni zinaonesha kuwa Schulz hawezi kuchukua nafasi ya Markel.

No comments:

Post a Comment