Sunday, September 3

Marekani yaikashifu Korea Kaskazini kwa kufanya jaribio la bomu la nyuklia

Trump: matamshi na vitendo vya Korea Kaskazini ni hatari kwa MarekaniHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionTrump: matamshi na vitendo vya Korea Kaskazini ni hatari kwa Marekani
Marekani imejiunga na nchi zingine kuikashifu Korea Kaskazini baada ya nchi hiyo kufanya jaribio la bomu la nyuklia.
Korea Kaskazini ilisema kuwa ilifanikiwa kulifanyia majaribio bomu la hydrojeni, ambalo linaweza kuwekwa kwenye kombora la masafa marefu.
"Matamshi ya nchi hiyo na vitendo vyake vinandelea kuwa vyenye hatari kubwa kwa Marekani," Rais Donald Trump aliandika kwenye mtandao wa twitter.
Korea Kaskazini imekaidi vikwazo vya Umoja wa Mataifa na shinikizo za kimataifa za kuitaka iache kuunda silaha za nyuklia zilizoweza kufika nchini Marekani.
Korea Kusini, Japan, China na Urusi ya wamelikashifu vikali jaribio hilo la sita la bomu la nyuklia lililofanyw na Korea kaskazini
Trump amezilaumua China na Korea Kaskazini kuhusu jinsi zinavyoishughulikia Korea Kaskazini.
"Korea Kaskazini imekuwa tisho na uibu kwa China," ambaye ni mshirika wake na ambaye amekuwa na mafanikio kidogo katika kupata suluhu.
"Matamshi ya kufurahisha ya Korea Kusini kwa Korea Kaskazini hayatafaulu," Trump alisema.
Wakati huo huo watu kwenye mji mkuu wa Korea Kaskazini Pyongyang, wanaendelea kufahamu hatua ya nchi yao ya kulifanyia jaribio bomu la nyuklia.
Watu hao walipiwa picha wakisherehekea hatua hiyo.
Watu hao walipiwa picha wakisherehekea hatua hiyo.Haki miliki ya pichaALAMY
Image captionWatu hao walipiwa picha wakisherehekea hatua hiyo.
Watu hao walipiwa picha wakisherehekea hatua hiyo.Haki miliki ya pichaALAMY
Image captionWatu hao walipiwa picha wakisherehekea hatua hiyo.
Watu hao walipiwa picha wakisherehekea hatua hiyo.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWatu hao walipiwa picha wakisherehekea hatua hiyo.
Watu hao walipiwa picha wakisherehekea hatua hiyo.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWatu hao walipiwa picha wakisherehekea hatua hiyo.

No comments:

Post a Comment