Kiongozi wa Islamic State huenda yuko hai, kwa mujibu wa afisa wa cheo cha juu wa jeshi la Marekani na kukinzana na madai ya Urusi kuwa huenda ilimuua wakati wa uvamizianchini Syria mwezi Mei.
"Abu Bakr al-Baghdadi huenda amejificha katika eneo lililo kati ya Iraq na Syria," alisema jenerali Gen Townsend.
Huenda alikimbia ngome za Islamic State ambazo zimekuwa chini ya mashambulizi kutoka pande zote mbili.
Mahali alipo Baghdadi hapajulikani.
Mwezi Juni Urusi ilisema kuwa kulikwa na uwezekano kuwa Baghdad, alikuwa ameuawa mapema kwenye shambulizi la angani lililofanywa na Urusi mjini Raqqa.
Tangu wakati huo makundi yanayopinga kundi la Islamic tatate yamefanya mashambulizi katika mji huo ambapo takriban wapiganaji 2000 bado wako.
Baghdadi aliaminika kuwa mjini Mosul kabla ya muunganoa unaongozwa na Marekani kuznzisha jitihada za kuukomboa mwezi Oktoba.
Ameonekana hadharani mara moja tu miaka ya hivi karibuni kwenye video akihubiri mjini Mosul tare 5 Julai mwaka 2014.
Nayo kanda ya video kumhusu ilitolewa mwisho tarehe 2 Novemba mwaka uliopita.
No comments:
Post a Comment