Wakazi hao hutembea umbali wa kilometa 68 kufuata huduma ya matibabu katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema.
Kauli hiyo aliitoa juzi katika mkutano wa hadhara uliokuwa na lengo la kuhamasisha maendeleo wakati akiwahutubia wakazi wa Kata ya Bupandwa jimboni hapo.
“Niamini, kazi yangu kubwa kwenu ni kuwaletea maendeleo, kikubwa ninachowaomba tushirikiane kwa pamoja,” alisema.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa, Crispin Luanda alisema suala la maendeleo halina mjadala hivyo kinachotakiwa ni usimamzi uliotukuka kufikia maendeleo hayo.
Mmoja wa wakazi wa Kata ya Bupandwa, Juma Kazimili alisema kwamba mafaniko yote yanayopatikana yanatokana na juhudi na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na viongozi wa jimbo kutokana na fedha zinazotumwa kufanya kazi iliyokusudiwa.
No comments:
Post a Comment