Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, amasema hayo leo mkoani Morogoro wakati akifungua maonyesho ya 26 ya wakulima, Nanenane, kanda ya Mashariki yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.
Profesa Maghembe amesema ili kuwawezesha wakulima kuzalisha kwa tija, ni vyema mbegu za GMO zikatumika ili kuwawezesha wakulima kuzalisha kwa wingi na kuondokana na umasikini.
Aidha, Waziri Maghembe amesema nchi sasa inatakiwa kubadilika kifikra na kukubali kama ambavyo nchi nyingine za Afrika na Asia zimefanya.
Amesma nchi hizo zimepata mafanikio makubwa baada ya kukubaliana na mabadiliko hayo.
Aliyolea mfano wa yuzalishaji wa pamba ambalo limeanza kutumia mbegu hizo za GMO na na wakulima kuanza kupata mafanikio.
Amesema kwa mbegu za GMO za z pamba zianze kutumika, zimekuwa na tija kwa wakulima ukilinganisha mbegu ziliokuwa zikitumika zamani, ambapo mbegu hizo zinatoa mazao bora, mengi na yanayohimili ukame na wadudu, ambapo mazao yake yamekuwa na soko kubwa.
Amepongeza namna watafiti nchini wanavyobuni mbegu zinayohimili ukame, akitolea mfano wa mbegu aina ya mahindi ya wema inayohimili ukame, wadudu na zinazostawi maeneo mengi hapa nchini.
“Kumekuwa na masuala ya ujima na imani potofu kuhusiana na mbegu hizi, lakini mimi kama mtaalamu wa kilimo na utafiti nawaeleza tuwasikilize watafiti na wataalamu wetu kwani kila kitu kinabadilika na tunaendelea kuwaumiza wakulima,” amesema.
Waziri huyo alisema hakuna budi kwa serikali sasa kupanga bei elekezi ya mazao, sambamba na kuisimamia baada ya wakulima kuvuna mazao yao ili kuepuka ulanguzi .
Katibu tawala wa mkoa wa Morogoro Cliford Tandari alisema hadi sasa kanda ya mashariki imefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh 80 milioni na matarajio kufikia Sh140 milioni na hiyo ni baada ya Serikali kuamua kuchukua jukumu la kuendesha shughuli za maonyesho ya wakulima kutoka kwa chama cha wakulima Tanzania (Taso) kilichokuwa kikiratibu maonyesho hayo.
Tandari alisema pamoja na ukusanyaji huo wenye mafanikio lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutokuwepo kwa uzio kwa baadhi ya maeneo hivyo kupoteza fedha nyingi.
Pia alitaja changamoto nyingine kuwa ni uhaba wa maji katika uwanja huo sambamba na Taso kuuza maeneo ya maonyesho hayo kwa matumizi ya makazi kinyume na utaratibu.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe, amewataka watu wote waliouziwa viwanja katika uwanja huo kinyume na utaratibu wakiwamo ambao tayari wameshajenga makazi ya kudumu, kuondoka mara moja.
No comments:
Post a Comment