Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Viwanda, Charles Mwijage wakati akiwasilisha taarifa ya mkutano wa SADC uliomalizika hivi karibuni na kujadili hali ya viwanda na biashara kwa nchi za Afrika.
Waziri Mwijage amesema kuwa Tanzania itaweza kunufaika kwa ajili ya zao la alizeti kwa kuongeza mauzo katika soko la kimataifa.
Ameongeza kuwa SADC pia imeitaka Tanzania kuweka mpango wa miaka mitatu kwa ajili ya uzalishaji wa sukari ili kuweza kufikia tani laki 8.
Mwijage amewataka wote wenye mashamba na waliopewa mashamba kwa ajili ya kilimo cha miwa wahakikishe wanalima kilimo chenye tija kwa manufaa ya viwanda vyetu.
No comments:
Post a Comment