Tuesday, August 22

Mahakamani kwa kula nyama ya mtu


Durban.Watu wanne  wamefikishwa mahakamani nchini Afrika Kusini kujibu mashtaka ya kula nyama ya binadamu.
Aidha, watu hao wanakabiliwa pia na mashitaka ya kupanga mauaji.
Watu hao walibainika baada ya  mmoja wao kujipeleka katika kituo cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama ya binadamu.
Alipohojiwa zaidi mtuhumiwa huyo alionyesha sehemu ya mguu na mkono wa binadamu ambavyo vilisalia baada ya kula sehemu nyingine za mwili.
Kisha polisi wakaandamana na mtuhumiwa  huyo mpaka kwenye  nyumba moja iliyopo katika mji wa KwaZulu-Natal na kushuhudia  miili mingine ya watu.
Kati ya watu hao wanne, wawili ni waganga wa jadi..

No comments:

Post a Comment