Saturday, August 5

Wadau wataka mfumo wa mitihani utazamwe upya


HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani imehimizwa kuzingatia umuhimu wa kutenga asilimia moja ya mapato ya ndani kwa ajili ya kukabili changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu.
Hayo yalisemwa na Methew Chungu ambaye ni mwezeshaji wa mafunzo yaliyoandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (Shivyawata) Kibaha Mjini kwa wadau wa huduma za afya kwa watu wenye ulemavu.
Chungu alisema mapato hayo yatasaidia kuwapatia huduma mbalimbali watu wenye ulemavu zikiwemo za kiafya, elimu, kiuchumi na huduma nyingine za kiutu. Katibu wa Sivyawata Kibaha Mjini, Happiness Matagi alisema kwa sasa changamoto za upataji huduma kwa watu wenye ulemavu zimepungua ambapo kumwona daktari ni bure.
Matagi alisema kupitia kituo chao cha watu wenye ulemavu kilichopo Kwa Mfipa, wanatoa huduma mbalimbali zikiwamo za kiafya hasa kwa watu wenye ulemavu wa viungo pamoja na shughuli za ujasiriamali.
“Pale watu wenye ulemavu wanafanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufuma, kushona nguo na mradi wa matofali ambao uko mbioni kuanza lengo kuwakwamua watu wenye ulemavu ili wasijione wanyonge na hivyo, waachane na tabia ya kuombaomba ambayo itawafanya washindwe kujitegemea,” alisema Matagi.
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Dk Mariamu Mgaya alisema watu wenye ulemavu wamekuwa wakisaidiwa kwa namna mbalimbali ili kuhakikisha wanapata huduma za afya bila usumbufu kwa kuwapa kipaumbele.
Akijibu baadhi ya hoja, Ofisa Mipango wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Amkauane Ngilangwa alisema katika bajeti iliyopitishwa, watu wenye ulemavu wametengewa Sh milioni 10. Alisema pia wanapatiwa vitu mbalimbali ikiwamo mafuta ya kuwasaidia watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) ili ngozi zao zisiharibike, pamoja na fimbo kwa ajili ya wasioona.

No comments:

Post a Comment