Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bw. Deodatus Alexander akimkabidhi kitambulisho chake Bw. Abrahman Mohamed Mussa, akiwa miongoni mwa wananchi waliokamilisha taratibu za Usajili na kukabidhiwa Vitambulisho vyao wakati wa maonyesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Ngongo Lindi.
Baadhi ya wananchi wakikamilisha taratibu za Usajili kwa kuchukuliwa alama za vidole, picha na saini ya Kielektroniki wakati wa maonyesho yanayoendelea Viwanja vya Ngongo Lindi.
Wananchi wa Manispaa ya Lindi wakipata maelezo ya taratibu za Usajili toka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi.Rose Mdami wakati maonyesho ya Nanenane yakiendelea mkoani Lindi.
Wananchi wakiendelea kusubiria kupata huduma ya Usajili kwenye banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) mkoani Lindi.
Bi Khadija Khalid mtaalamu wa mifumo ya Komputa mkoani ofisi ya NIDA Lindi, akitoa elimu kuhusu mfumo wa Utambuzi na Usajili wa Taifa kwa wananchi waliofika kujifunza kwenye Banda la NIDA.
Baadhi ya wananchi wakisubiri kupata huduma kwenye banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wakati wa maonyesho ya Kilimo Nanenane yanayoadhimishwa kitaifa mkoani Lindi.
Maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakiendelea kutoa huduma kwa wananchi waliofika kutembelea Banda la Mamlaka hiyo viwanja vya Ngongo Lindi.
Hawa ni baadhi tu ya wananchi wakihakikiwa na Afisa wa Idara ya Uhamiaji Bw.Kudrack Kuvagwa kabla ya kuchukuliwa alama za Kibaiolojia, picha na Saini ya Kielektroniki.
No comments:
Post a Comment