Monday, August 7

MTANZANIA ALPHONCE SIMBU ASHIKA NAFASI YA TATU MBIO ZA DUNIA JIJINI LONDON



MTANZANIA Alphonce Felix Simbu amefanikiwa kunyakua medali ya Shaba baada ya kushika nafasi ya tatu katika mbio za dunia za IAAF zinazoendelea kufanyika nchini Uingereza katika Jiji la London.
Simbu ameshika nafasi ya tatu nyuma ya Mkenya aliyeshika nafasi ya kwanza akifuatiwa na Muethiopia aliyeshika nafasi ya pili.
Akitumia masaa 2 na dakika 10 Simbu aliweza kushika nafasi ya tatu baada ya kumpita Mkenya mwingine aliyekuja kushika nafasi ya tano.
Hii inakuwa ni kwa mara ya kwanza kwa Simbu kushika nafasi ya tatu baaada ya mwaka jana katika mbio ndefu za  London Marathonaliweza kushika nafasi ya tano.

No comments:

Post a Comment