Ridhiwani amesema kuwa aliwahi kuambiwa na mzee huyo kuwa anatamani kumuona anakua kijana mwenye mapenzi kwa vijana wenzake.
Ndesamburo aliwahi kuwa mbunge wa Moshi mjini kwa tiketi ya Chadema na pia mwenyekiti wa chama hicho hadi alipofariki dunia dunia miezi michache iliyopita.
Ridhiwani amesema hayo baada ya kwenda kuhani msiba nyumbani kwa marehemu mjini Moshi.
Akizungunza na baadhi ya ndugu na jamaa marehemu Ndesamburo, Ridhiwani amesema alikutana mara ya kwanza ana kwa ana na kuzungumza na mzee huyo miaka kadhaa iliyopita alipokwenda Moshi kumuona babu yake aitwaye Mzee Semindu na pia alikutana naye tena kipindi cha Bunge la Katiba.
"Namkumbuka sana, aliwapenda sana wabunge vijana na hata akiwaona wamekuwa kimya sana aliwauliza kuwa vipi mbona uko mpole leo?” amesema
No comments:
Post a Comment