Saturday, August 26

Ofisi ya mawakili Dar yashambuliwa


Dar es Salaam. Mlipuko unaosadikiwa kuwa wa bomu umeharibu ofisi za wanasheria za kampuni ya IMMMA zilizopo Barabara ya Umoja wa Mataifa jijini hapa.
Mlipuko huo umeelezwa kutokea usiku wa kuamkia leo Agosti 26 na umeharibu ofisi hizo zilizoko eneo la Upanga.
Miongoni mwa wamiliki wa kampuni hiyo ni Fatma Karume, ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.
Kwa sasa Barabara ya Umoja wa Mataifa iliyokuwa imefungwa tangu asubuhi imefunguliwa na polisi wanaendelea na uchunguzi ndani ya jengo la ofisi hiyo. Pia kuna magari mawili ya polisi na moja la zimamoto.
Baadhi ya nyumba zilizo jirani na ofisi hiyo imeelezwa zimevunjika vioo na kuharibika paa.







No comments:

Post a Comment