Akizungumza mara baada yakutoka nje ya kituo Kikuu cha Polisi wakili wake Peter Kibatala amesema Lissu ameachiwa kwa dhamana na atatakiwa kurudi tena Jumatatu.
Baada ya kutoka nje ya kituo cha polisi Lissu hakutakiwa kuzungumza chochote kutokana na masharti ya dhamana badala yake aliingia moja kwa moja kwenye gari ya wakili wake.
Kibatala amesema Lissu anatuhumiwa kutoa maneno ya uchochezi pamoja na kumkashfu Rais.
No comments:
Post a Comment