Port Arthur ni miongoni mwa maeneo ambayo yanashuhudia mafuriko makubwa mno
Mlipuko umeripotiwa kutokea katika kiwanda kimoja cha kemikali karibu na mji wa Houston nchini Marekani mahali ambapo janga la mafuriko ya maji yametokea.
Vyombo vya habari nchini Marekani vinaripotio kuwa mashuhuda wamesiki milipuko miwili mikubwa imetokea huku moshi mweusi ukionekana ukifuka kutoka kiwanda cha kemikali cha Arkema kilichoko mjini Crosby.
Wakati wa mvua kubwa iliyotokana na kimbunga cha Harvey, kiwanda hicho kilipoteza uwezo wa kutia barafu katika sehemu yake ya iliyo na kemikali, ambayo inafaa kuwa baridi suku zote.
Awali kampuni hiyo ilionya kuwa hakukuwa na njia ya kuzuia kutokea kwa mlipuko huo.
Yamkini watu 33 wamefariki katika janga hilo la kimaumbile, ambalo idara ya Kitaifa ya hali ya hewa nchini Marekani, imeweka kimbunga hicho katika kiwango cha chini cha upepo tu.
Ni nini kilichofanyika katika kiwanda hicho cha kemikali?
Kiwanda cha kemikali cha Arkema, kiko maili 21 kutoka mji wa, na kilifungwa siku ya Ijumaa muda mfupi kabla ya kimbunga hicho kugonga maeneo hayo.
Lakini mvua iliyosababisha mafuriko ya kina cha inchi 40 (102cm) katika maeneo hayo, yamesababisha mafuriko makubwa na kusababisha kukatika kwa umeme. Hayo ni kwa mjibu wa taarifa ya habari kutoka katika kampuni hiyo.
Mitambo ya jenereta pia yamezamishwa majini.
Kiwanda hicho kinaunda kemikali ya organic peroxides, kemikali inayotumika kuundia karibu kila kitu kama vile dawa, hadi vifaa vya ujenzi, ambayo inaweza kuwa hatari zaidi wakati wa joto jingi.
"Joto ya aina yoyote inaweza kusababisha kulipuka kwa gesi," Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Richard Rowe, ameliambia shirika la habari la Reuters.
Mvua kubwa inatarajiwa kuendelea kunyesha huko Louisiana hadi Kentucky siku tatu zijazo, huku tahadhari ya kutokea kwa mafuriko zaidi ikiendelea kutatiza maeneo ya Kusini Mashariki mwa jimbo la Texas na maeneo ya Kusini Magharibi mwa Louisiana.
Usambazaji wa umeme nchini Marekani umetatizwa, huku kampuni ya mafuta ikifunga viwanda vya kusafisha mafuta na mabomba makubwa ya kupitishia mafuta katiika mji wa Houston na viunga vyake.
Maafisa wa zima moto watafanya msako wa nyumba hadi nyumba hasa katika maeneo ambayo yaliathirika pakubwa na mafuriko hii leo Alhamisi, ili kuwaokoa manusura ambao wangali wamekwama pamoja na kuopoa maiti ya watu waliofariki kutokana na janga hilo.
Siku ya Jumanne, Houston ilitangaza tahadhari ya kuzuia waporaji kuingia katika nyumba za watu ambao wameacha nyumba zao baada ya kuhamishiwa maeneo salama.
Tahadhari kama hiyo pia ikatolewa siku ya Jumatano katika mji wa Port Arthur.
No comments:
Post a Comment