Mwanasheria wa mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Shukuru Khalifa alisema mteja wake alikamatwa mchana alipokuwa akiandaa banda hilo.
“Anasema akiwa Chongoleani wakati akiendelea na maandalizi, alipigiwa simu na mkuu wa polisi wa Wilaya ya Tanga akiulizwa yuko wapi, alipojibu alipo baada ya muda mfupi alifuatwa na askari akapelekwa kituo cha Chumbageni” alisema Shukuru. Mwanasheria huyo alisema alipokwenda katika kituo hicho kwa ajili ya kumdhamini alizuiwa kwa madai kwamba mwanamke huyo anadaiwa kufanya biashara eneo ambalo haliruhusiwi.
Shukuru alisema anadhani mteja wake alikamatwa baada ya vyombo vya dola kujenga hisia kwamba anaweza kuandaa bango ili kulionyesha kwa Rais Magufuli kama alivyofanya jijini Dar es salaam.
“Ukweli ni kwamba Swabaha hakuwa na nia ya kumwendea Rais, alikwenda kuweka banda ili afanye biashara kama ilivyo kwa wengine na alifuata taratibu zote akaruhusiwa,” alisema Shukuru.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba alipotafutwa kuelezea tukio hilo simu yake iliita bila kupokewa.
No comments:
Post a Comment