Wazazi wa msichana mwenye umri wa miaka 13 mhasiriwa wa matendo ya ubakaji kutoka mji wa Mumbai huko India, wamekwenda katika mahakama kuu ya nchi hiyo, kuomba idhini ya kuavya mimba aliyo nayo binti wao.
Msichana huyo ana mimba ya wiki 30.
Sheria nchini India, inakubalia uavyaji mimba wa wiki 20 ikiwa tu maisha ya mwenye mimba iko hatarini.
Mimba hiyo iligunduliwa baada ya wazazi wake kumchukua kwa daktari kwa matibabu, kutokana na kuongezeka uzito kupita kiasi.
Msichana huyo anasema kuwa alibakwa na rafiki wa babake, ambaye kufikia sasa amekamatwa na kuzuiliwa.
Kesi hiyo inafanyika siku kadhaa baada ya msichana mwengine mhasiriwa wa ubakaji mwenye umri wa miaka 20, alipozaa katika mji ulioko Kaskazini mwa India wa Chandigarh.
Masaibu yake yalisababisha hisia kubwa kote duniani huku vyombo vya habari vikiangazia pakubwa taarifa hiyo, hasa baada ya mahakama kukatilia mbali ombi la kuavya mimba hiyo kwamba mimba hiyo ilikuwa ni kubwa mno kwa kuavya.
Mwezi Mei, kesi kama hiyo iliripotiwa katika mji wa Hyarana kaskazini mwa India, ambapo msichana mwenye umri wa miaka 10 ambaye alidaiwa kubakwa na babake wa kambo, alikubaliwa kuitoa mimba hiyo.
Mwaandishi wa BBC mjini Delhi huyo India, Geeta Pandey, anasema kuwa kesi tatu kama hiyo, imewashangaza wengi, lakini wanaharakati wanaamini kuwa, kuna uwezekana wa visa vingi kama hivyo, ambavyo haviripotiwi na vyombo vya habari, kwa sababu vinagundfuliwa baada ya makataa ya majuma 20 na wazazi wengi waharipoti visa kama hivyo kwa polisi.
No comments:
Post a Comment