Monday, August 28

Gurmeet Ram Rahim Singh, amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela na mahakama India

Polisi India wanasema kuwa wamepewa idhini ya "kuwapiga risasi na kuuwa" ni amri wakati wa ghasiaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionPolisi India wanasema kuwa wamepewa idhini ya "kuwapiga risasi na kuuwa" ni amri wakati wa ghasia
Mahakama moja kaskazini mwa India imemhukumu Guru mmoja wa kidini mwenye utata kifungo cha miaka 10, kwa kosa la kuwabaka wanawake wawili.
Juma lililopita, mahakama hiyo ilimpata na hatia Bw. Gurmeet Ram Rahim Singh, anayejiita mtu mtakatifu na makosa ya kuwabaka wanawake hao wawili, ambao ni waumini wake.
Hukumu yake ilisababisha ghasia na maandamano mabaya katika majimbo ya Haryana na Punjab ambapo watu 38 waliuwawa.
Maelfu ya polisi wa kupambana na fujo, wametumwa karibu kila mahali nchini India ili kuzua vurumai na ghasia ambazo zinaweza kutokea.
Taarifa zaidi zingali zikitokea.
Gurmeet Ram Rahim Singh pia huimba nyimbo za Rock
Image captionGurmeet Ram Rahim Singh pia huimba nyimbo za Rock
Walinda usalama kote nchini India, wamewekwa katika hali ya tahadhari, kabla ya mahakama nchini humo kutoa uamuzi wa mwisho katika hukumu ya ubakaji dhidi ya kiongozi mmoja wa kidini.
Wafuasi wa Gurmeet Ram Rahim Singh, walizua vurumai na ghasia siku ya Ijumaa, baada mahakama moja mjini Panchkula kumshitaki guru huyo.
Watu 38 waliuwawa katika ghasia hizo.
Amri ya kutotoka nje usiku imewekwa katika majimbo mawili ya Haryana na Punjab, ilihali usalama mkubwa ukiimarishwa katika mji mkuu Delhi.
Wanajeshi wa taifa hilo pia wako katika hali ya tahadhari, huku polisi wakisema kuwa wamepewa idhini ya "kuwapiga watu risasi na kuuwa" sheria inayotumika wakati wa matatizo.
Bw. Singh, mwenye umri wa miaka 50, hakupelekwa mahakamani kusomewa mashtaka dhidi yake, badala yake jaji aliyemhukumu, alipelekwa kwa ndege hadi gereza la Rohtak, anakozuiliwa Guru huyo, ili kumhukumu huko.
Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu mchana, saa za Afrika Mashariki.
Gurmeet Ram Rahim Singh ni nani?
Gurmeet Ram Rahim
Image captionGurmeet Ram Rahim
  • Kiongozi huyo mwenye utata, wa madhehemu ya Dera Sacha Sauda sect, inayodai kuwa na zaidi ya wafuasi milioni 60 kote Duniani.
  • Alianza kuongoza madhehebu hayo- inayodai kuwa "isiyohitaji faida bali inayoshughulikia maslahi ya kijamii na kiroho".
  • Anaigiza katika tasha za muziki aina ya Rock, kuigiza kwenye filamu na pia kuwa na msururu wa bidhaa zake za chakula.
  • Anajulikana kama "rockstar baba" na "guru of bling" kutokana na mavazi yake yanayomeremeta.
  • Ameshutumiwa mara kwa mara kwa kuwakejeli viongozi wa madhehebu ya Sikh na Hindu.
  • Amekuwa akichunguzwa kwa kosa la mauwaji na ubakaji, makosa ambayo ameyakanusha.
  • Ameshutumiwa kwa kuwalazimisha wafuasi wake wa kiume kuhasiwa ili "kukaribia zaidi mungu"
Polisi akimkabili mmojawepo wa wafuasi wea madhehebu ya Dera Sacha Sauda nchini India
Image captionPolisi akimkabili mmojawepo wa wafuasi wea madhehebu ya Dera Sacha Sauda nchini India
Gereza anamozuiliwa Guru huyo imefanywa kuwa ngome, huku waandishi wa habari wakizuiwa kulifikia kwani wanazuiliwa umabli wa kilomita 1.5 au kama (maili moja) mraba.
Mji wa Rohtak ulioko katika Jimbo la Haryana, pia unalindwa na maafisa wa polisi na jeshi, huku barabara zote zikiwekwa sen`genge ya miiba.
Idadi kubwa ya polisi wamezingira boma la Bwana Singh lililoko katika ekari 1,000 huko Sirsa, Haryana.
Shule na vyuo vimefungwa, huduma za simu za mkononi zimekatwa kote Haryana tangu Alhamisi iliyopita, huku marufuku hiyo ikiongezwa kwa masaa 48 yajayo.
Mamia kwa maelfu ya wafuasi wake wanaamini wangali ndani ya makao yake makuu ya madhehebu hayo ya Dera Sacha Sauda, huku baadhi yao wakiamua kuondoka kutokana na taharuki ya uwepo wa polisi.

No comments:

Post a Comment