Thursday, August 24

Makurutu washauriwa kutopiga punyeto China

Jeshi la taifa hilo limekuwa likishindwa kupata maafisa wapya katika miaka ya hivi karibuni licha ya kuwapongeza wanajeshi wake kuwa wazalendo.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJeshi la taifa hilo limekuwa likishindwa kupata maafisa wapya katika miaka ya hivi karibuni licha ya kuwapongeza wanajeshi wake kuwa wazalendo.
Jeshi la China limewapatia ushauri makurutu wanaotaka kujiunga nalo kuhusu watakavyotakiwa kupita vipimo vya maungo hatua iliosababisha mzaha miongoni mwa watumiaji wa mitandao.
Katika chapisho la mtandao, Jeshi hilo limeshutumu utumiaji wa kupita kiasi wa vinywaji vyenye gesi, uchezaji michezo ya kompyuta na hata kupiga punyeto kama vyanzo vya afya mbaya miongoni mwa vijana .
Imesema kuwa viipimo vya maungo miongoni mwa vijana wengi vimeshuka huku nusu ya wawaniaji wa kazi hizo katika mji mmoja wakifeli.
Jeshi la taifa hilo limekuwa likishindwa kupata maafisa wapya katika miaka ya hivi karibuni licha ya kuwapongeza wanajeshi wake kuwa wazalendo.
Ushauri waliopewa ni:
Ushauri huo ulionekana katika mtandao wa jeshi wa WeChat unaofanana na ule wa WhatsApp mnamo tarehe 19 mwezi Agosti.
Ulionyesha data kutoka mji mmoja wa China ambapo asilimia 56.9 wa vijana waliokuwa wakiwania kazi hizo walifeli kimaungo na kutoa ushauri kwa wanaowania kazi hizo kufuata maagizo 10 muhimu.
  • 1.Kupunguza unywaji wa pombe: Takriban asilimia 25 ya makurutu walifeli vipimo vya damu na mikojo.
  • 2.Tumia muda mchache katika runinga: Asilimia 46 ya makurutu walifeli vipimo vya kuona ambapo jeshi linalaumu utumiaji wa kupitia kiasi wa simu za rununu mbali na vifaa vyengine vya kielektroniki.
  • 3.Fanya mazoezi zaidi: Asilimia 20 ya makurutu walifeli kwa kuwa walikuwa wanene kupitia kiasi.
  • 4.Punguza michezo ya kompyuta pamoja na kupiga punyeto: Asilimia nane walifeli kutokana na uharibifu katika sehemu zao za siri kutokana na kuketi kwa muda mrefu.
  • 5.Jifunze kulala kwa muda: Asilimia 13 ya makurutu walifeli kwa kuwa walikuwa na shinikizo la damu.
  • 6.Usijiweke tatoo
  • 7.Kunywa maji safi: Asilimia 7 walifeli kutokana matatizo ya masikio, pua na koo kutokana na kunywa maji yasio safi.
  • 8.Kufanyiwa matibabu ya magonjwa yanayopitishwa kupitia jeni: Asilimia 3 ya makurutu walifeli kutokana na kutokwa na jasho jingi mwilini .
  • 9.Tafuta tiba ya magonjwa ya kiakili: Asilimia 1.6 walifeli kwa sababu ya maswala ya kiakili hususan shinikizo la kiakili.
  • 10.Kuwa msafi: Asilimia 3.4 ya makurutu walifeli kutokana na magonjwa ya kieneo.
Chapisho hilo lilivutia mzaha huku maelfu ya watu wakiingia katika mtandao wa Weibo kujadili swala hilo.
''Mwaka ujao watataka makurutu kutahiriwa'' , alisema mtumiaji mmoja.
Mtumiaji mwengine alisema ''anashuku kuwa na alama ya kuzaliwa pia ni tatizo kubwa''.
''Kwa nini kuna watu wengi wasio na afya nzuri''?, mtumiaji mmoja aliuliza.
Wengine waliuliza kwa nini watu wanafeli kwa kutoona vizuri.

No comments:

Post a Comment