Thursday, August 24

Korea Kaskazini 'yafichua makombora' yake kimakosa

Kim Jong-un katika shule ya ulinzi na sayansi akikagua vifaa .Picha hiyo ilionyesha makombora ya Hwasong 13 na Pukguksong-3.Haki miliki ya pichaKCNA
Image captionKim Jong-un katika shule ya ulinzi na sayansi akikagua vifaa .Picha hiyo ilionyesha makombora ya Hwasong 13 na Pukguksong-3.
Korea Kaskazini imeonekana kufichua maelezo ya makombora yake mawili ambayo hayajafanyiwa majaribio katika mkutano wake na wanahabari kukagua kiwanda chake.
Ukaguzi huo ulifanywa na kiongozi wa taifa hilo Kim Jong-un.
Picha zilizochapishwa na chombo cha habari cha taifa hilo KCNA ili kuandamana na ripoti kuhusu ukaguzi huo wa kim Jong-un katika shule ya ulinzi na sayansi zinaonyesha chati ilioelezea kuhusu makombora ya Hwasong 13 na Pukguksong-3.
Kombora la Hwasong 13 linaonekana kuwa na awamu tatu {ICBM} huku chati hiyo ikionyesha kuwa kombora la Pukguksong-3 ni la manuwari ya kivita SLBM.
Sio mara ya kwanza kwamba Korea Kaskazini imefichua siri zake kwa bahati mbaya kupitia picha, na hilo huenda linaonekana kuwa ni njia mojawapo ya kuonyesha ubabe wao wa kijeshi ama hata kutuma ujumbe kwa wapinzani wao.
Image caption
Ripoti hiyo ya ukaguzi inaonekana kufanyika wakati ambapo kumefanyika zoezi la pamoja la kijeshi kati ya Korea Kusini na Marekani ambapo Pyongyang inapinga.
Muda wa ukaguzi huo na yalioonekana ni muhimu.
Akizungumza na gazeti la JoongAng Iibo, afisa wa ulinzi na maswala ya usalama katika eneo la Korea Shin Jong-woo alisema kuwa Korea kaskazini ina historia ya kuonyesha makombora yake ama hata picha kupitia vyombo vya habari vya taifa ili kudhihirisha ubabe wake wa kijeshi duniani.
Kulingana na chombo cha habari cha KNCA, Kim Jong un anasemekana kuagiza wanasayansi katika kiwanda hicho kutengeza roketi za vichwa vya makombora na hayo ni sawa na maelezo yalionekana katika chati.
Ikilinganisha na kombora la Hwasong 14 ambalo Korea Kaskazni ilifanyia majaribio mnamo mwezi Julai, Hwasong 13 linaonekana kuwa kombora la awamu tatu huku lile la Pukguksong 3 likiwa kombora la masafa marefu la makombora ya Pukguksong 1 na 2 ambayo yalijaribiwa 2016.
Image caption
Iwe makosa ama iwe makusudi imefanyika hapo awali.
Wiki mbili zilizopita, picha za Kim Jong-un akipanga kurusha kombora katika maji ya kisiwa cha Guam nchini Marekani pia zilionekana katika chati mbali na kambi ya kijeshi ya Guam.
Ujumbe uko wazi.
Pyongyang inaiambia Washington kwamba uwezo wa jeshi la Marekani katika eneo hilo uko taabani.
Pyongyang imekuwa ikitumia mbinu za kutishia wakati wa wasiwasi.
Mnamo mwezi Machi 2013 rais Kim Jong-un alipigwa picha akiwa na majenerali waliobeba vipatakilishi baada ya eneo hilo kuonekana kuelekea kutumbukia katika vita kufuatia jaribio la kombora mwezi mmoja uliopita.
Chati moja ilionyesha mpango wa kutaka kushambulia Marekani, huku kombora moja likilenga eneo la Austin huko Texas.
Image caption
Kama njia ya kutishia, mpango huo haukufanikiwa huku habari za tishio hilo zikifanyiwa mzaha na watumiaji wa mtandao wa Twitter mjini Texas .
Na huku Korea Kaskazini ikionekana kukosa uwezo wa kutekeleza shambulio kama hilo, ingekuwa vigumu kwa taifa hilo kutekeleza mpango huo hata iwapo ingetaka kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment