Kusogezwa mbele kwa kesi hizo ni baada ya mawakili upande wa Jamhuri kuomba tarehe zingine kwa upelelezi wa mashauri hayo haujakamilika.
Malinzi na wenzake wanashtakiwa kwa makosa 28 yakiwemo ya kugushi na utakatishaji fedha.
Wakati kesi ikipangwa kusomwa tena Agosti 11, upandwa wa viongozi wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Geoffrey Kaburu zimepigwa kalenda hadi Agosti 7.
Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa alisema kesi hiyo Aveva na Nyange inahitaji upelelezi wa muda mrefu kutokana na asili ya mashitaka yake.
"Mahakama haina mamlaka ya kuifuta kwa siku 60, hivyo wanatoa tarehe fupi ili upande wa mashitaka ufanye kazi ya kukamilisha upelelezi."
Miongoni mwa mashitaka yanayowakabili Aveva na Kaburu ni pamoja na kughushi nyaraka zinazodaiwa kuwa klabu ya Simba inawalipa madeni watuhumiwa hao kiasi cha dola za Kimarekani 300,000.
Makosa mengine ni Aveva kutoa nyaraka za uongo kwa Benki ya CRDB Tawi la Azikiwe Dar es Salaam Machi 10, 2016, la tatu ni kutakatisha fedha kinyume cha sheria, ambapo inadaiwa rais huyo na Kaburu walikula njama za kufanya uhalifu huo.
Shtaka la nne ni Kaburu kutakatisha fedha dola 300,000 na kuziweka katika Benki ya Barclays Tawi la Mikocheni mjini Dar es Salaam, na la tano ni kutakatisha fedha likimhusu tena, Makamu wa Rais, Kaburu anayedaiwa kumsadia Aveva kutakatisha fedha katika benki ya Barclays baada ya kughushi nyaraka.
No comments:
Post a Comment