Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Jumatatu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jafari Mohamed alisema kuwa tukio hilo lilitokea Julai 30 majira ya saa 11:15 jioni katika kitongoji cha Kitaramanka, Kata ya Mirwa.
Alisema baada ya marehemu kutoka matembezini alifika nyumbani moja kwa moja na kuingia bafuni kitendo kilichomkasirisha mkewe akidai kwanini amerudi na kuingia bafuni moja kwa moja.
Kamanda Mohamed alisema kuwa baada ya marehemu kuambiwa hivyo walianza ugomvi na mpenzi wake huyo, katika purukushani za hapa na pale ndipo Jeni alipomchoma na kitu chenye ncha kali upande wa titi la kushoto na kusababisha kifo chake.
Kamanda alisema mtuhumiwa ameshakamatwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara kwa uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment