Thursday, August 31

Injini ya pikipiki kubeba tani moja ya mzigo


Dar es Salaam. Katika kuadhimisha siku ya wahandisi, bidhaa za ubunifu likiwemo gari la kubeba mizigo litakalotumia injini ya pikipiki zitaonyeshwa.
Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Injinia Patrick Balozi amesema maadhimisho hayo yatafanyika Septemba 7 na 8 mjini Dodoma.
Amesema gari hilo lina uwezo wa kubeba mzigo wenye uzito wa tani moja.
Bidhaa zingine za ubunifu zitakazoonyeshwa ni mashine ya kushindilia katika ujenzi wa barabara, ya kuchakata migomba ili kutengeneza nywele bandia na ya kusaga mihogo.
Amesema shughuli zitakazofanyika kwenye maadhimisho hayo ni majadiliano ya kitaaluma, kuwatambua na kuwazawadia wahandisi waliohitimu masomo mwaka 2016/17 na maonyesho ya kazi za wahandisi.
Kaimu msajili amewaomba waajiri kuwaruhusu na kufadhili ushiriki wa wahandisi ili waweze kushirikiana na wenzao katika ujenzi wa viwanda.

No comments:

Post a Comment