Thursday, August 31

DStv yashusha bei ya vifurushi

Dar es Salaam. Kampuni ya Multichoice Tanzania imeshusha bei ya vifurushi kuanzia kesho Septemba Mosi.
Kwa uamuzi huo, sasa wateja wataweza kushuhudia Ligi Kuu ya Uingereza kupitia Super Sport 3 na ligi nyingine kwa Sh69,000 kwa mwezi ndani ya kifurushi cha Compact badala ya Sh82,250 za awali.
Taarifa ya kampuni hiyo imesema kifurushi cha Compact plus kitakuwa Sh109,000 badala ya Sh122,500 za awali huku cha Premium kikishushwa bei kutoka Sh184,000 hadi Sh169,000 kwa mwezi.
Kifurushi cha Family kimeshushwa bei kutoka Sh42,900 hadi Sh39,000, huku cha Bomba kikishuka kutoka Sh19,975 hadi Sh19,000 kwa mwezi.

No comments:

Post a Comment