Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart inatarajia kupiga mnada jengo la Abla Complex lenye urefu wa ghorofa saba lililopo Mikocheni Dar es Salaam kutokana na mmiliki wake kushindwa kulipa mkopo anaodaiwa na KCB Bank Limited.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bi. Scholastica Kevela, Yono wataendesha Mnada huo August 12, 2017 hapo hapo mjengoni, na amekaribisha yeyote mwenye nia ya kununua jengo afike kwenye mnada huo kuanzia saa nne na nusu asubuhi (From 10.30 am).
No comments:
Post a Comment